
Baadhi ya watuhumiuwa hao yupo Afisa mtendaji wa Kata ya Lengatei Julias Kirato, Afisa mtendaji wa Kijiji cha Engong’ongare Ndatoya Chang’idi, Meneja wa Msiti wa mbao SULEDO Isaya Saitabau na wengine 7
Miongoni mwa walioshtakiwa katika kesi ya watu hao 10 walioharibu mali na wizi wa fedha taslimu na bidhaa mbalimbali ni pamoja na Afisa mtendaji wa Kata ya Lengatei, Julias Kirato, Afisa mtendaji wa Kijiji cha Engong’ongare Ndatoya Chang’idi, na Meneja wa Msitu wa mbao Suledo Isaya Saitabau na wananchi wengine 7
Watu hawa kwa pamoja wanatuhumiwa makosa mbalimbali yakiwemo kukata matairi ya trekta na kuweka chumvi kwenye injini, kuiba mafuta ya deasel lita 120, kuiba fedha taslimu na simu dukani pamoja na bidhaa mbalimbali kisha kuchoma moto vibanda vya wakulima katika Kijiji cha Engong’ongare.
Akisoma mashitaka hayo Mwendesha mashtaka wa Serikali Mkaguzi msaidizi wa Polisi Joseph James aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Julias Kirato Afisa mtendaji wa Kata ya Lengatei, Ndatoya Chang’idi Afisa mtendaji wa Kijiji cha Engongongare, Isaya Saitabau Meneja wa Msitu wa mbao Suledo.
Wegine ni Yohana Olunyaji, Sumail Lemongo, Nyerubo Nyenasi,Leboi Kitui, Ndatuya Tang'idi na Saigori Mgaya
Alisema watuhumiwa hawa wanakabiliwa na mashtaka 14 waliyatenda kwa pamoja Desemba 30.2022 katika Kijiji cha Engong’ongare Kata ya Lengatei, yakiwemo makosa ya wizi kinyume na kif cha 258 na 265 cha sheria, kosa la kuharibu mali kif cha 326 (1) sura ya 16 ya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja kwa nia ovu waliteketeza trekta namba T 738 DWM aina ya Soraji kwa kukata matairi na kuweka chumvi kwenye Injini, kuiba fedha taslimu, kuiba vitu vya dukani zikiwemo simu za aina mbalimbali, vinywaji kisha kuteketeza kwa moto vibanda vya wakulima na kuungua vitu mbalimbali zikiwemo fedha taslimu
Watuhumiwa hawa 10 kwa pamoja baada ya kusomewa mashtaka yao 14 wamekana ambapo imeelezwa mahakamani hapo kuwa dhamana yao iko wazi kwa kila mshtakiwa awe na wadhamini wawili akiwa na mafungu tofauti ya fedha kulingana na makosa hayo tofauti