Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema "ameshtushwa" na utekaji nyara katika "shambulio la kwanza la aina hii linalowalenga wanawake kwa makusudi" nchini Burkina Faso.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema ina wasiwasi mkubwa.
msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price alisema katika taarifa yake kwamba Wale waliotekwa lazima warejeshwe salama kwa wapendwa wao mara moja na bila masharti, na wale waliohusika wanapaswa kuwajibishwa kwa kiwango kamili cha sheria.
Katika taarifa yake, Ufaransa imelaani utekaji nyara huo na kutoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa wanawake hao.
Hakuna kundi lililosema lilihusika na utekaji nyara huo lakini utekaji nyara ulifanyika katika eneo ambalo wanamgambo wanaendesha harakati zao

