Ijumaa , 11th Mar , 2016

Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene amesema kuwa ucheleweshaji wa mafao umekua ukizidisha ugumu wa maisha kwa wastaafu na kusababisha migogoro kati ya wastaafu na serikali hivyo ameiagiza mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa mafao kwa wakati.

Waziri wa TAMISEMI Mhe. George Simbachawene

Akizungumza katika Mkutano mkuu wa LPF unaoendelea jijini Arusha ,Simbachawene ameitaka mifuko hiyo kuhakikisha kuwa wastaafu wengi nchini wanakabiliwa na msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili baada ya kustaafu wanashindwa kujimudu kutokana na kukosa mafao yao.

Mhe. Simbachawene amesema kuwa kitendo cha kuwacheleweshea mafao yao ni kuonyesha dhahiri kutokuthamini mchango wa wazee hao kati umri wa ujana wao katika kulijenga taifa hivyo wengi wao hubaki kuichukia Serikali.

Aidha waziri huyo wa TAMISEMI ameongeza kuwa Wazee wengi wanaonekana kuichukia serikali kutokana na mifuko hiyo kutokufanya kazi zake ipasavyo kitu ambacho kinapelekea chuki dhidi ya serikali iliyopo madarakani