
Wanachama hao kutoka vyama vya CUF na CHADEMA, wamekabidhi kadi zao kwa Waziri wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Matambarare Kusini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
Akiwa katika kijiji cha Matambare Kusini, Waziri Mkuu amepokea wanachama 17 ambao kati yao 13 wanatoka Chama cha Wananchi (CUF) na wanne wanatoka Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA). Katika kijiji cha Ng’au kata ya Mnacho, Majaliwa amepokea wanachama wawili wa (CHADEMA).
Kwa upande mwingine Waziri Mkuu ambaye yupo kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka anaendelea na ziara ya jimboni kwake kwa kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji miche bora na mipya.