Jumapili , 6th Dec , 2015

Serikali mkoani mara imeagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali zikiwemo za kisheria mtu ama kikundi cha watu ambacho kitabinika kukwamisha oparesheni ya usafi wa mazingira kama ilivyotangazwa na Rais Dkt. John Magufuli

Mkuu wa mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu wa jeshi la wananchi Aseri Msangi

Mkuu wa mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu wa jeshi la wananchi Aseri Msangi,ametangaza agizo hilo wakati wakazi wa manispaa ya Musoma na wilaya ya Rorya vikiwemo vikosi vya ulinzi na usalama vikishiriki katika zoezi la mazingira kwa nyakati tofauti katika wilaya hizo mbili.

kwa upande wao baadhi ya wananchi na viongozi wa maeneo hayo,pamoja na kumpongeza rais kwa kuwakumbusha watanzania kuhusu wajibu wao katika zoezi hilo ambalo linalenga kupambana na ugonjwa wa kipindupindu,

Aidha wananchi hao pia wamezitaka halmashauri kutunga sheria ndogo ambazo zitawezesha zoezi hilo kuwa la kudumu badala ya kungojea agizo la rais kila mwaka