Jumanne , 17th Jan , 2023

 Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ,wamechimba shimo na kudumbukia kwenye  duka la simu eneo la Kitengela huko nchini Kenya.

Majambazi hao wamefanikiwa kuiba bidhaa zenye thamani isiyopungua shilingi milioni 13 za Kitanzania.

Kamera za ulinzi ziliweza kunasa tukio hilo, ambapo anaonekana kijana mmoja akitoboa ukuta na kisha kuzima kamera moja, huku akimruhusu mwenzake kuingia ndani, tukio lililojiri kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 12 asubuhi.

Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo lililojiri tarehe 12 mwezi huu, huku polisi wakiendelea na uchunguzi.