Baadhi ya wahudumu wa mochwari
Wahudumu wa vyumba vya kuhifadhia maiti mortuary wa hospitali mbalimbali hapa nchini wakiongea na EATV baada ya kuhitimu mafunzo ya mochwari yanayotolewa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, wamesema ipo haja ya kitengo hicho kutiliwa maanani kwa kutoa ujuzi husika kwa wanao fanya kazi hiyo pamoja na ajira rasmi.
Akiongea kwa niaba ya Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Muuguzi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Claudia Kaluli, amesema serikali inaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya uboreshaji yanayotolewa.