Jumatano , 27th Dec , 2017

Msanii wa Bongo Fleva Saleh Ali maarufu  kama Ali Kiba amewaomba radhi mashabiki wake na kuwaahidi kufungua mwaka kwa kishindo kufuatia kushindwa kufanya  tamasha la Funga Mwaka na King Kiba.

Ali Kiba aliahidi kufanya tamasha hilo lengo likiwa ni kuwafikia mashabiki wake wanaompa sapoti, ambapo amekuwa na utaratibu huo wa kufanya matamasha kwa ajili ya kuwafikia mashabiki wake wanaomsapoti katika kazi yake ya muziki.

Msanii huyo amekuwa na mafanikio makubwa mwaka huu baada ya kushinda tuzo mbili za AFRIMA kupitia nyimbo yake ya Aje ambayo ilishinda tuzo ya nyimbo bora ya RNB & SOUL na Aje remix aliyomshirikisha MI Abaga wa Nigeria ambayo ilishinda tuzo kama nyimbo bora ya kushirikiana.

Mkali huyo wa Bongo Fleva anaetamba na wimbo wake wa Seduce Me, aliahidi kufanya  tamasha la funga Mwaka na King Kiba ambalo alitarajia kulifanya nchini nzima.