Ijumaa , 16th Mei , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Desire Luzindah ameendelea kujifua ili kuboresha muziki wake kwa njia ya kufanya maonesho ya Live na bendi, na imefahamika kuwa kwa sasa anaendelea kujifua kwa mazoezi makali.

Desire Luzindah

Ili kuthibitishia mashabiki wake kuwa amedhamiria kufanya mabadiliko makubwa, Desire ameamua kumuajiri msanii mkali wa kupiga gitaa, Myco Ouma kuungana na timu inayopiga live muziki wake, na kwapamoja wamekuwa wakijifua katika swala la muziki wa live.

Desire ni moja kati ya wasanii wakubwa kabisa Uganda ambao kwa aina ya muziki wanaoufanya, mashabiki wao wamekuwa kwa kiasi kikubwa wakiwataka kubadilika na kufanya maonesho live ili kuleta uhai na uhalisia zaidi kwa kazi zao.