
mashindano ya dance100% 2014 Tanzania
Gumzo hili kubwa limetokana na burudani na umahiri mkubwa ambao umekuwa ukionyeshwa na washiriki katika mashindano hayo kwa mashabiki.
Hili limedhihirika hasa kutoka katika rekodi za makundi 5 yaliyofanikiwa kupenya kuingia hatua ya Nusu Fainali The WT, Wakali sisi, Best Boys, Wazawa Crew na The winners Crew, ambao mitindo yao kudansi, ushirikiano kama kundi na ubunifu ndivyo vilivyoweza kuwafanikisha kujivunia maksi nyingi kutoka kwa majaji.
Msisimko unaongezeka kuelekea fainali ya mashindano haya Jumamosi ya tarehe 4 Oktoba, ambapo ushindani utakuwa mkali zaidi kutokana na uwezo wa makundi haya, swali kubwa likiwa ni kundi gani litaibuka washindi wa mashindano hayo kwa mwaka huu.