Jumatano , 23rd Jul , 2014

Msanii wa muziki Iryn Namubiru, ametangaza kusitisha shughuli zake za kimuziki, ikiwepo tukio la uzinduzi wa video zake mpya ili kupisha shughuli za msiba wa mtoto wa pekee wa msanii Juliana Kanyomozi, Keron ambaye atazikwa Ijumaa hii.

mwanamuziki wa Uganda Iryn Namubiru

Iryn ambaye amekuwa moja ya wasanii waliokuwa mstari wa mbele kupeleka ujumbe wa Faraja kwa Juliana, amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, uzinduzi wa video hii utafanyika katika tarehe ambayo ataitangaza baadaye baada ya msiba kumalizika.

Mwili wa marehemu Keron tayari umekwishafikishwa nchini Uganda jana ukilakiwa na umati mkubwa wa waombolezaji ambao pia walitarajia kumuona Juliana katika msafara huo na kumpatia pole bila mafanikio kutokana na msanii huyo kutoonekana kabisa.