Alhamisi , 21st Oct , 2021

Producer Claud wa ngoma ya doa ya msanii Liah ambaye anadai kuibiwa verse na melody za wimbo huo na Alikiba, anasema hawezi kujua ni nani aliyemuibia mwenzake wimbo huo, hivyo Liah na Tommy Flavour ndio wanaoujua ukweli.

Kulia ni picha ya msanii Alikiba, kushoto ni Liah

Liah anasema wimbo wake umekopiwa na Alikiba kupitia ngoma ya sitaki tena inayopatikana kwenye Album ya Kiba 'Only One King' huku muandishi wa ngoma hiyo ni Tommy Flavour.

Zaidi mtazame hapa kwenye video akitoa maelezo kuhusu sakata hilo.