Jumamosi , 30th Jan , 2016

Kayumba, msanii wa muziki ambaye anatokea katika mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba, amesema kuwa ana uhakika wa kuvunja historia iliyopo ya wasanii waliopitia njia kama yake kutokufanya vizuri, akiweka imani yake juu ya uongozi alionao.

Kayumba

Kayumba ambaye yupo chini ya Mkubwa na Wanawe ameeleza kuwa, wenzake wameweza kuyumba kutokana nakukosa usimamizi thabiti, tofauti na yeye ambaye kwa kuanzia tayari amekwishakamilisha project kubwa kabisa huko Afrika Kusini, akiwa katika matayarisho ya kufanya uzinduzi mkubwa kabisa wa kazi yenyewe katika viwanja vya wazi maeneo ya Temeke.

Kayumba ameweka wazi pia juu ya kufanikiwa kuwa mmiliki wa gari alilolipata muda sio mrefu, ikiwa ni moja ya mafanikio yake makubwa kimuziki.

Tags: