Jumatatu , 31st Oct , 2016

Baada ya mrembo Diana Edward kutoka Kinondoni jijini Dar es salaam kutangazwa mshindi wa taji la 'Miss Tanzania' na kuandamwa na maneno kwenye mitandao, watu mbalimbali wajitokeza kumtetea mrembo huyo mwenye asili ya kimasai.

Miss Tanzania 2016 Diana Edward (katikati aliyekaa) akiwa na warembo waliotinga tano bora.

 

Watu hao ambao pia ni maarufu hapa nchini  wamepost kwenye mitandao yao ya kijamii huku wakionesha 'surport' yao kwa mlimbwende huyo anayetokea kwenye jamii ya kimasai, ambaye ameandamwa na jamii wakidai amependelewa na hakustahili kushinda taji hilo, huku wakisema ndiye hasa anayefaa kubeba taji hilo na wana imani atapeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye mashindano ya urembo wa dunia. (Miss World)

"When You Nailed that question Properly, I knew that The Crown was Yours.... Congratulations mdogo wangu... You deserve it... And I have a very good feeling about Your performance in the Miss World Beauty Pageant.... You will do Tanzania Proud", aliandika Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kushinda taji hilo mwaka 2006.

Pia muigizaji wa filamu kutoka bongo, Kulwa Kikumba au Dude ameandika haya...."Tumpe nafasi Miss Tanzania, nimepita mitandaoni nimeona akisemwa vibaya sana, na hivi ni binti mdogo alipo atakuwa kapata hofu sana, atapoteza kujiamini, najua hakuwahi kuwaza kukutana na hili, huo ndiyo ubaya wa umaarufu, tumpe nafasi pengine akafanya vizuri kuliko waliotangulia, kila la kheri mmasai wetu".

Naye mke wa aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii Faraja Kota Nyalandu ambaye naye alishawahi kushinda taji hilo mwaka 2004, ameandika ujumbe wa kuwataka watanzania kuwa na upendo na kuacha kumshambulia binti huyo, huku akikumbusha aliyoyapitia baada ya yeye kushinda taji hilo na uchungu alioupata.