"Mama yangu alinyanyaswa, mpaka amefariki "-Shetta

Jumamosi , 23rd Mei , 2020

Moja kati ya wasanii wenye maisha mazuri  hapa Bongo ni Shetta, pia kwa sasa msanii huyo anashirikiana na sekta za Serikali kufanya kazi kama msafara wa kijinsia kumtokomeza ukatili chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Msanii Shetta

Sasa Shetta ameisanua show ya Friday Night Live ya East Africa TV jinsi alivyopata mchongo huo wa kushirikiana na Serikali kufanya kazi kwenye sekta kama hizo.

"Watu wasichukulie hili ni tobo la kutokea unatakiwa ufanye  kwa manufaa ya jamii, kwanza nina stori ya kuwaeleza watu kwamba mama yangu alipitia manyanyaso kutoka kwenye familia kabisa mpaka amefariki 2006 alikuwa amepitia hayo mambo ambayo mimi  kama mtoto yalinisababishia matatizo na kukosa vitu vya msingi shuleni na mavazi" amesema Shetta 

Zaidi na zaidi tazama kwenye video hapa chini