
Siku ambayo Chidy Designs alimvalisha pete ya uchumba msanii wa filamu Jacqueline Wolper
Akidhibitisha hilo wakati anazungumza na waandishi wa habari Chidy Designs amesema "Labda niweke wazi mimi na Jack tulikuwa mtu na mchumba wake, katika wanawake ambao nimewahi kuwa nao amewazidi baadhi ya vitu kwa sababu anajua kuitafuta pesa kwa jasho lake mwenyewe na ameweka kazi mbele".
"Kutokana na mazingira ambayo yupo nayo na mimi kazi zangu zinavyoenda, unakuta kuna vitu havipo sawa halafu mwisho wa siku kila mmoja kivyake, kuna kitu kimeingia na hakipo sawa baada ya pete ya uchumba tumeachana" ameongeza.
Huko nyuma Jacqueline Wolper aliwahi kuwa na mahusiano na Dallas, Harmonize, Official Brown, Young Killer na kwenye mahojiano ya msanii wa singeli Meja Kunta ameweka wazi kwamba alikuwa na mahusiano naye.