Muna Love atafsiri maana ya sebene la Yesu

Jumatano , 24th Jun , 2020

Mtumishi wa Mungu Muna Love, amesema maana ya sebene la Yesu ni ujumbe wa Mungu ambao anautumia kwa njia ya kucheza nyimbo za masebene na disko, yanayoambatana na maneno ya kumsifu na kumtukuza.

Mtumishi wa Mungu Muna Love

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Muna Love amesema atatumia kila njia ili kumtangaza Yesu kwa sababu, hata huko kuna madisko na masebene pia yupo kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa sababu Mungu amemtendea vitu vingi.

"Maana ya sebene la Yesu ni ujumbe wa Yesu unaoambatana na maandiko ya Mungu, nina mapatano yangu na Mungu kwamba nitamtangaza kwa kila njia ili mradi hata asiyesoma atakusikia, kwa Mungu kuna kila kitu kuna vibe, disko, masebene, kuabudu na kusifu mimi nipo kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa sababu amenitendea vitu vingi na hapo bado sijacheza sebene maana nitacheza sana" amesema Muna Love.