
Rose amesema, kwa mtu yoyote kuendelea katika nafasi aliyopo ni muhimu kujituma kujifunza zaidi kwa upande wa sekta binafsi na sekta rasmi, ikiwa inafahamika pia kuwa elimu haina mwisho.
Staa huyo amekuwa mfano wa kielelezo baada ya kufanikisha siku ya jana kuingiza mtaani rasmi jarida lake ambalo linafahamika kwa jina Rozzie, likiwa na taarifa na dondoo mbalimbali za kuelimisha na kuburudisha, hatua ambayo ni ya mafanikio makubwa pembeni na nafasi yake kama msanii wa maigizo.