Neno la Odama kwa wadangaji wa BongoMovie

Ijumaa , 20th Mar , 2020

Moja kati ya tasnia ambayo inaongoza kwa kutuhumiwa na ishu za udangaji ni BongoMovie, lakini muigizaji Odama amesema hiyo ni tabia ya mtu binafsi, siyo lazima awe maarufu au atokee kwenye tasnia yao.

Msanii wa filamu Odama

Odama amefunguka hayo kwenye show ya eNewz ya East Africa TV, ambayo inaruka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 12:00 hadi 12: 30 jioni, ambapo amesema

"Mimi naamini kila mtu ana tabia yake, kabla hata hujaingia katika kazi ambayo sisi tunaifanya kila mtu huingia na tabia yake aliyokua nayo, kwahiyo wale wote ambao wamegeuka kuwa na tabia ya kudanga, basi huo ndiyo uhalisia wao tangu zamani na wote wenye tabia nzuri hawajabadilika" ameeleza Odama.

Msanii huyo wa filamu ameendelea kusema "BongoMovie haichangii watu kudanga ili kuonekana maisha yao yapo juu, inawezekana hata mtu asiwe na jina, ustaa, umaarufu lakini ukadanga  wanaodanga wote kwenye filamu walikuwa wanataka wapate nafasi ili waonekane wafanye mambo yao" ameongeza.