Jumanne , 14th Apr , 2015

Ney wa Mitego, moja ya wasanii wanaofanya vizuri katika game ya muziki Bongo, amezungumzia utaratibu wa mauzo ya muziki kwa njia ya mtandao ambayo imeanza kushika kasi kwa sasa.

msanii wa bongofleva nchini Ney wa Mitego

Ney amesema kuwa kutokana na kukatishwa tamaa hapo awali, kwa upande wake hajawahi kufuatilia maslahi na faida ya mfumo huo.

Mkali huyo ameongezea kuwa, baada ya migogoro na pia kupata malipo kidogo licha ya kuwa na ngoma kali katika mfumo wa caller tunes, ameamua kutokufuatilia masuala haya ya kiteknolojia katika muziki wake.