Jumatano , 5th Oct , 2016

Rapa Young Killer ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake 'Mtafutaji' amefunguka na kujigamba kuwa wimbo utakaofuata baada ya kazi yake hii ni hatari na kusema yeye mwenyewe anapousikiliza wimbo huo anauogopa kutokana na namna alivyoufanya.

Young Killer

Young Killer amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo kilichokuwa kinaruka moja kwa moja kutokea Kawe Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa mashabiki wakae mkao wa kula kuja kusikia kazi hiyo.

"Nawashukuru sana mashabiki zangu kwa kuendela kunipa 'Support' katika kazi yangu mpya 'Mtafutaji' lakini nawaahidi kuwa kazi yangu mpya inayofuata ni hatari sana mimi mwenyewe nikiisikiliza kazi hiyo naogopa, hivyo wasubiri tu wakati wake ufike watashuhudia wenyewe" alisema Young Killer