
Petii amfunguka hayo kwenye Friday Night Live (FNL) ya East Africa Television, na kusema kwamba ni kweli amemaua kuoa kimya kimya, na sasa ameona bora aweke wazi kutokana na maswali mengi kutoka kwa watu mbali mbali.
“Maneno yamekuwa ni mengi sana, suala la msingi nakubali ni kweli nimeoa, I have a ring kwenye kidole changu”, amesema Petii.
Petii hakuishia hapo bali aliendelea na kuweka wazi juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kati yake na msanii wa bongo fleva, Karen, na kusema kuwa wawili hao hawakuwa wapenzi, na hata sare walizokuwa wakivaa ilikuwa ni mavazi tu kwa kawaida na sio kwa ajili ya mahusiano.
“Karen alikuwa rafiki yangu tu, nilikuwa namsapoti sana kwenye kazi zake kwa sababu mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye ile kazi, sasa ilinibidi, kuhusu kuvaa sare mimi naweza nikanunua nguo mbili hata na Jolie akavaa”, amesema Petii.