Jumatatu , 3rd Jul , 2017

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmiliki  wa lebo ya 'Switch Music Group' (SMG), Quick Rocka amefunguka kwamba changamoto za mapenzi zinazowakabili wasanii wa kike ndiyo sababu ya mpaka leo lebo yake kukosa msanii wa jinsia hiyo.

Quick Rocka ametaja mahusiano kama moja ya sababu zinazopelekea ugumu huo na kusema iwapo 'member' yeyote wa OMG akiwa na mpenzi ambaye ni msanii anaweza akapata nafasi katika lebo hiyo kwa kuwa wivu hautakuwepo, huku  akionya kuwa endapo watashindwana hapo ndipo ugumu unazidi.

“Ni vigumu sana kumsimamia msanii wa kike coz kuna vitu vingi hasa anapoanza kuingia kwenye mahusiano, labda yeye ana mtu wake sisi tupo on tour au kuna zile usiku mnene studio, unajua ule wivu wa hapa na pale unaweza ukamzuia asi-perform vizuri katika codes,”  Quick Rocka alifunguka

Lebo ya SMG hadi sasa ina wasanii wanne waliotoka ambao ni Quick Rocka na member wa watatu wa kundi la OMG, na sasa hivi wanatamba na wimbo wao ‘Watasema’.