'Ray aligeuka baba wa watoto waliokomaa' - Chuchu

Alhamisi , 16th Mei , 2019

Mwigizaji kutoka Bongo Movie, Chuchu Hansy amefunguka kuhusu mzazi mwenzake Vicent Kigosi (Ray), kuwa baada ya kupata mtoto wao aitwaye Jaden, Ray alijiona baba mpaka wa watoto waliokomaa.

Vicent Kigosi Ray na Chuchu Hansy

Chuchu amefunguka hilo leo kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati akimtakia heri ya siku ya kuzaliwa mzazi mwenzake huyo.

Happy Birthday baba @jadenthegreatest baba mwenye jeuri zako baada ya kupata mtoto ukajiona baba mpaka kwa watoto wakubwa waliokomaa.

Lakini Chuchu ameweka wazi kuwa hana tatizo na Ray na kusisitiza hivi, ''No matter what nakutakia Happy Birthday Mungu azidi kukuweka inshaalah uje mleane na mwanao sina zawadi kubwa zawadi yangu ni @jadenthegreatest na natumai ni zawadi ya milele na yenye historia kwako''.