
Kwenye picha kulia ni Young Killer, kushoto Young Lunya
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Salmin Swaggz amesema kuna watu wa kushindana nao kwenye game, pia huwezi kushindana na kila mtu.
"Kuna watu wakushindana nao kwenye game na sio kila mtu lazima ushindane naye, paka hawezi kudisiwa na panya halafu akajibu lakini ninachomaanisha sio kwamba Young Killer ni paka halafu Young Lunya ni panya hapana ni vitu tofauti, Young Killer alijitengenezea ukubwa wake ila Young Lunya ndiyo wakati wake kwa sasa" ameeleza Salmin Swaggz
Pia amefunguka kuhusu mustakabali wa kundi la OMG kwa kusema halijavunjika na mipango inaendelea japo kila mtu anafanya kazi kivyake ila muda sio mrefu wataachia kazi mpya ambayo itawakutanisha wasanii wote wa kundi hilo ambao ni Young Lunya, Conboi, na Salmin Swaggz.