Jumanne , 13th Mei , 2014

Katika jitihada za kuhakikisha kuwa wasanii hapa nchini Tanzania wanatengenezewa mazingira mazuri zaidi ya kufaidika na kazi wanazotengeneza, Serikali imeagiza COSOTA na Mamlaka ya Mapato TRA, kukutana ndani ya siku za kazi kuanzia sasa.

Mhe Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi

Mpango huu ni kwaajili ya kutengeneza makubaliano juu ya mfumo utakaofaa kwa ajili ya kukusanya na kudhibiti mapato ili kuboresha faida kwa wasanii na serikali.

Agizo hili limetolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa kipindi cha maswali na majibu, baada ya Mbunge Mhe. Martha Mlata alipotaka kujua hatua ambazo Serikali inachukua kuhakikisha kuwa mapato yanayokusanywa kutoka kwa wasanii yanafaidisha pande zote mbili.