Jumapili , 23rd Aug , 2015

wasanii mbalimbali nchini wakiwemo wa muziki na filamu kwa pamoja leo hii wamejumuika kutumbuiza katika uzinduzi wa kampeni za urais, ubunge na udiwani za Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wasanii wa muziki na filamu wakiungana katika uzinduzi wa kampeni ya CCM Kitaifa.

Wasanii hao wakiwemo Peter Msechu, Yamoto Band, Diamond, Bushoke, Dokii, Hafsa Kazinje, Ruby, Hadija Kopa na
wengineo walitoa burudani ya aina yake katika uzinduzi huo ambao umeweza kuwakusanya umati wa watu wengi akiwemo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DK Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kutoka nchini Tanzania.