
Young D
Hata hivyo Young D amesema hajawa na taarifa yoyote kutoka katika uongozi wake kuhusiana na taarifa rasmi ya kufanya video hiyo kwa kuwa walikuwa wakishughulikia kwanza swala la kumbadilisha muonekano wake wa zamani na kumuweka sawa.
Pia hakusita kuushukuru uongozi wake kwa kumtoa katika hali ya zamani aliyokuwa nayo ya matumizi ya madawa ya kulevya na anashukuru Mungu kwa sasa anaendelea vizuri.