Jumatatu , 30th Dec , 2019

Mtandao wa WhatsApp hautofanya kazi kwenye simu janja zinazotumia mfumo wa Window 'Window Smartphone' kufikia Disemba 31, kwa mujibu wa mtandao wa Mirror.

WhatsApp

Mtandao huo unaotumiwa na mabilioni ya watu hivi sasa, una mpango wa kuondoa huduma hiyo kwenye simu janja za makampuni mengine wiki za hivi karibuni.

Simu zitakazoathirika katika miezi ya hivi karibuni ni pamoja na baadhi ya simu janja za Android pamoja na baadhi za iPhone.

Simu za Android toleo la 2.3.7 hazitakuwa na uwezo wa kutengeneza akaunti mpya au kuboresha (update) akaunti zao za zamani ifikapo Februari 1.

Pia simu za iPhone zinazofanya kazi kwenye mfumo wa iOS 8 pia hazitaweza kutengeneza akaunti mpya au kuthitisha akaunti zao za zamani ifikapo tarehe hiyo.

"Hautakuwa na uwezo wa kutumia WhatsApp kwenye simu janja zinazotumia mfumo wa Window baada ya Disemba 31, 2019, pia WhatsApp inaweza isipatikane kwenye 'Microsoft app store", ulisema uongozi wa mtandao huo.