Jumanne , 10th Sep , 2019

Klabu ya soka ya Azam FC imefikia makubaliano ya kuingia mkataba mpya wa miaka miwili zaidi na kiungo mshambuliaji, Richard Djodi.

Mchezaji Richard Djodi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'

Djodi amesaini mkataba huo mpya leo Jumanne mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'. Mkataba huo utamfanya kuendelea kusalia Azam Complex kwa miaka mitatu, hadi mwaka 2022.

Uongozi wa Azam FC umeamua kuingia naye mkataba mpya ndani ya muda mfupi, baada ya Djodi kufanikiwa kuonyesha kiwango kizuri katika mechi mbalimbali za mashindano, hali ambayo imemvutia Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, aliyependekeza kurefushwa zaidi kwa mkataba wake.

Nyota huyo raia wa Ivory Coast aliyesajiliwa akitokea Ashanti Gold ya Ghana, ambapo hadi sasa katika mechi tatu za mashindano alizoichezea Azam FC, amefunga mabao mawili.