Jumanne , 20th Dec , 2022

Klabu ya soka ya Azam FC imefikia makubaliano ya kuachana na mchezaji Ibrahim Ajib baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya klabu hiyo.

Ibrahim Ajib akiwa Azam FC

Ibrahim Ajib alijiunga na Azam FC, Disemba 30, 2021 kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine akitokea klabu ya Simba.

Tetesi pia zinaeleza kuwa mchezaji huyo ananukia kujiunga na klabu ya Singida Big Stars yenye maskani yake mkoani Singida.