Alhamisi , 4th Jul , 2019

Frank Lampard ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa Chelsea, kwa mkataba wa miaka mitatu, akitokea klabu ya Derby County ambayo ilicheza 'Play off Final' ya kuingia EPL lakini ikafungwa na timu ya Aston Villa ambayo kocha msaidizi ni mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea John Terry.

Frank Lampard

Lampard alijiunga na Chelsea Juni 2001 akitokea West Ham United. Lampard aliifunga goli lake la 200 akiwa na Chelsea tena kwa kuifunga klabu yake ya zamani West Ham Machi 17, 2013.

Lampard anashikilia rekodi ya kucheza mechi 164 mfululizo za ligi kuu ya England. Alifanya hivyo kati ya 13 Oktoba 13, 2001 Desemba 26, 2005.

Lampard ameichezea Chelsea kwa misimu 13. Mechi yake ya kwanza ilikuwa ni ya ligi kuu dhidi ya Newcastle United, ambayo ilipigwa Agost 19, 2001 na kuisha kwa sare ya 1-1. Mechi yake ya mwisho ndani ya Chelsea ilikuwa ni dhidi ya Norwich City, Mei 4, 2014 iliyomalizika kwa suluhu.

Muingereza huyo ameichezea Chelsea jumla ya mechi 648 ambapo kati yahizo mechi 593 alianza. Wachezaji pekee wanaomzidi kwa mechi ni  Ron Harris, Peter Bonetti na John Terry.

Lampard ndio mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo akiwa amefunga goli 211. Katika magoli hayo goli lake la kwanza alifunga kwenye mechi yake ya tano tu akiwa na Chelsea ambayo ilikuwa ni ya UEFA Cup dhidi ya Levski Sofia.