Guardiola atumia mechi 60 kuweka rekodi

Ijumaa , 12th Jan , 2018

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mara nne mfululizo kwenye ligi kuu soka nchini England EPL.

Kocha huyo raia wa Hispania ametwaa tuzo hiyo katika miezi ya Septemba, Oktoba, Novemba na Disemba hivyo kuweka rekodi hiyo ya pekee.

Guardiola amefanikiwa kuweka rekodi hiyo akiwa ameiongoza City katika michezo 60 ya ligi kuu soka nchini England katika msimu mmoja na nusu tangu awe kocha wa timu hiyo. Katika mechi hizo ametwaa tuzo hiyo mara tano.

Katika mwezi Disemba Man City imecheza mechi nane na kushinda mechi saba huku ikitoka sare mchezo mmoja dhidi ya Crystal Palace na kufunga mabao 19 katika mechi hizo.

Guardiola sasa amemuacha mpinzani wake Jose Mourinho ambaye tangu aanze kufundisha timu za EPL amefundisha mechi 272 na kutwaa tuzo hiyo mara tatu pekee.