Joash Onyango atamba kuelekea kariakoo Derby

Jumanne , 4th Mei , 2021

Beki  wa kati  Klabu ya  Simba Joash Onyango  wameweka wazi kwamba watapambana kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Mei 8, Uwanja wa Mkapa.

Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba, Joash Onyango akiwa mazoezini.

Nyota huyo ambae ni raia wa kenya,Joash   amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku akisema mchezo  utaonesha taswira nzima ya kutetea ubingwa wao VPL. 

"Kwetu sisi kila mchezo ni muhimu na kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu lakini naamini kwa namna ambavyo tumejiandaa kwanzia sisi wachezaji hivyo mashabiki waje kwa wingi".

Mchezo wao wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba hivyo Mei 8 utakuwa ni mchezo wa kusaka ushindi ili kujenga ufalme katika kusaka ubingwa wa ligi.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 25, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 hivyo mshindi wa mchezo huo atakuwa anajenga mazingira ya kuelekea ubingwa.