Ijumaa , 29th Jan , 2016

Kocha wa Timu ya majimaji FC ya Mjini Songea Kali Ongala amesema, hivi sasa hawezi kuzungumzia nafasi anayoihitaji kuwa katika ligi kuu bali anaangalia zaidi kubaki katika ligi kuu ya Soka Tanzania bara.

Kali Ongala, Kocha wa Majimaji FC

Ongala amesema, mechi dhidi ya JKT Ruvu hapo kesho ni mechi ambayo wanatakiwa kufanya vizuri ili kuweka nafasi kubwa kati ya timu yake ya Majimaji na JKT Ruvu ili ku jiweka katika nafasi nzuri.

Ongala amesema, wanasafari ndefu sana katika Ligi kuu na kazi ngumu hivyo ni jukumu la uongozi na Timu kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya ligi kuu japo timu ndogo ndogo shiriki za ligi kuu zina matatizo mengi na wanachokifanya ni kutatua matatizo yaliyopo.

Ongala amesema, kikosi chake kina wachezaji wazuri na hakujua kama kikosi cha Majimaji kina wachezaji wazuri ambao wana uwezo mzuri wa kucheza ligi japo wana matatizo madogo madogo ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho ili waweze kuwa wazuri zaidi.