Alhamisi , 26th Mei , 2016

Shirikisho la Soka Barani Ulaya Uefa limeipiga faini ya paundi 8,384 klabu ya soka ya Liverpool kutokana na kitendo cha mashabiki wake kuwasha miale ya moto kwenye mechi ya robo fainali ya Uropa Ligi dhidi ya Borussia Dortmund.

Hukumu hiyo inakuja siku moja baada wekundu hao wa Anfield kupigwa faini nyingine ya paundi 43,577 kutokana na ushangiliaji haramu na makosa mengine madogo madogo dhidi ya Manchester United.

Liverpool ilipoteza mchezo wa fainali kwa Sevilla, ambapo timu zote mbili zimeshitakiwa kwa ushangiliaji wa foju wa mashabiki zao, na kesi hiyo itasikilizwa na Uefa Julai 21 mwaka huu.