Jumanne , 15th Feb , 2022

Manchester United wanataraji kushuka dimbani saa 5:15 usiku wa Leo Februari 15,2022 kucheza dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa kiporo cha Ligi Kuu ya England kujaribu kutafuta ushindi ili kurudisha hali ya utulivu na kujiamini kwenye timu hiyo.

(Wachezaji wa Manchester united wakipasha misuli kabla ya mchezo.)

United walitoka sare michezo miwili mfululizo dhidi ya Burnley na Southampton michezo yote wakitangulia kufunga kisha kusawazishiwa na matokeo hayo yakaishusha toka nafasi ya nne hadi ya tano katika msimamo wa ligi kuu ya England.

Gwiji wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand amesema United hua wanacheza vizuri sana mwanzoni mwa mchezo, lakini baadae makosa binafsi ya wachezaji ndio yanaigharimu timu.

Naye kocha wa muda wa mashetani hao wekundu Ralf Rangnick amesisitiza kuwa hakuna haja ya kumvua unahodha Harry Maguire kama madai ya baadhi ya wadau na wachambuzi wanavyo shauri licha ya kukiri kwamba kweli ameona udhaifu kwa mlinzi huyo.