Alhamisi , 13th Oct , 2022

Mfadhili wa zamani wa klabu ya Simba, Azim Dewji amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze siku ya Jumamosi kuchangia damu ikiwa kama sehemu ya sadaka katika mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Premio De Agosto utaopigwa jumapili hii katika dimba la Benjamin Mkapa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dewji amesema mashabiki wajitokeze kwa wingi kuchangia damu kwani Tanzania bado inahitaji damu katika kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

''Mashabiki watakaojitokeza watapata tiketi zitakazowafanya waweze kuingia katika mchezo wa marudiano''amesema Dewji.

Zoezi hilo la kuchangia damu litafanyika Jumamosi katika hospitali ya Taifa Muhimbili saa 4:00 asubuhi.

Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 3-1 nchini Angola