
Mcheza tennis nambari mbili kwa ubora duniani muingereza Andy Murray atakutana uso kwa uso na mchezaji nambari moja mserbia Novak Djokovic katika fainali ya michuano ya wazi ya Australia.
Murray amefikia hatua hiyo baada ya kumtoa Milos Raonic katika hatua ya nusu fainali kwa jumla ya seti 3 kwa mbili 4-6, 7-5, 6-7, 6-4, 6-2.
Katika mchezo huo uliochukua zaidi ya saa 3, Raonic aliweza kumyumbisha Murray, kabla muingereza huyo hajacharuka na kupata ushindi katika seti mbili za mwisho.
Murray anakwenda kupambana na mbabe wake Djokovic, ambaye katika fainali tatu walizowahi kukutana, Djokovic amefungwa zote, na katika michezo 11 mfululizo iliyopita, Murray amepoteza michezo 10.
Murray anacheza fainali yake ya ya tano katika michuano hiyo ya Australia.
Mchezo huo wa fainali kati ya Murray na Djokovic utapigwa Jumapili huku fainali kwa upande wa wanawake Serena Williams atapambana na Angelique Kerber siku ya kesho.