Alhamisi , 29th Apr , 2021

Klabu ya soka ya Namungo FC kutoka Lindi, usiku wa jana Aprili 28, 2021, imepoteza mchezo wake wa mwisho dhidi Pyramids ya Misri kwa bao 1-0.

Steven Sey mshambuliaji wa Namungo aliyefanya vizuri katika mechi za kufuzu

Namungo ilionekana kuwakomalia wenyeji Pyramids hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, wakiwa suluhu 0-0 na hatimaye kumalizika kwa kupoteza bao 1-0 lililofungwa kunako dakika 64 na Ibrahim Adel.

Matokeo haya yameenda tofauti na mitizamo ya wengi, wapo walioamini Namungo FC wangefungwa magoli mengi kutokana na ubora wa Pyramids na kwakuwa walikuwa wanacheza nyumbani kitu kilichoenda kinyume.

Namungo FC ilikuwa kundi D lililoshuhudia Raja Casablanca ya Morocco na Pyramids ya Misri, wakifuzu katika hatua ya robo fainali kwa kuchukua nafasi ya kwanza na ya pili, huku Nkana ya Zambia wakiwa kwenye nafasi ya 3 na wao wakimaliza wa mwisho.

Takwimu za Namungo katika mashindano ya kombe la shirikisho CAF.
1. Raja Casablanca 1- 0 Namungo
2. Namungo 0- 2 Pyramids
3. Namungo 0-1 Nkana
4. Nkana 1-0 Namungo
5. Namungo 3-0 Raja Casablanca
6. Pyramids 1-0 Namungo