
Kocha Ralf Rangnick kushoto akiwa na Edinson Cavani
“Nilimwambia tangu siku ya kwanza, yupo kwenye mipango yangu na namuhitaji kwani yeye ni mchezaji pekee anayeweza kucheza kama mshambuliaji na kulitizama goli la mpinzani kwa hiyo nilimwmbia wazi kwamba namuhitaji abaki nasi na yeye anajua hilo na kwa jinsi gani ninavyompa heshima kubwa'' amesema Rangnick
Cavani raia wa Uruguayi ana umri wa miaka 34,alitoka benchi na kuisaidia Manchester United kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Newcastle United na kwenye mchezo uliopita aliisaidia tena kikosi hicho cha mashetani wekundu kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Burnley huku mkufunzi wa United Ralf Rangnick akiwa na kibarua kizito cha kutoa hatma ya nyota kama Anthony Martial, Jesse Lingard, Donny van de Beek na Paul Pogba.
Manchester United wapo nafasi ya saba wakiwa na alama 31 wakizidiwa alama 22 na vinara wa ligi Manchester city kwenye msimamo wa Epl na leo usiku wanacheza na Wolverhampton Wanderers ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu England ambayo ni Monday Night Football.