Jumapili , 30th Jan , 2022

Rafael Nadal wa Hispania akiwa na miaka 35, ameshinda Grand Slam ya 21 baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya wazi ya Australia kwa kumfunga mpinzani wake Daniil Medvedev.

Rafael Nadal

Nadal ameshinda fainali hiyo iliyopigwa leo Januari 30, 2022, Rod Laver Arena huko Melbourne  kwa jumla ya seti tano kwa tatu za 2-6 6-7 (5-7) 6-4 6-4 7-5. 

Nadal alianza vibaya dhidi ya Daniil Medvedev anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani, kwa kuwa nyuma kwa seti mbili kabla ya kurejea na kushinda.

Kutokana na ushindi huo wa leo, Nadal atapanda hadi namba moja kwenye viwango vya ubora wa mchezo huo duniani kwa upande wa wanaume akimshusha Novak Djokovic anayeshikilia nafasi hiyo.