
Akudo
Akiongea kupitia eNewz ya EATV amesema anajipanga kurudisha band ya Akudo na kuwaondoa wasanii wote wanaopenda kuwazoea wateja na kuwapiga vizinga hali inayopelekea mashabiki wengi kukimbia wakiogopa kuombwa hela na wasanii.
Yaani mtu akiingia ukumbini yeye ni pombe tu, yeye ni kuombaomba watu hela, hiyo nimeisimamia siitaki tena, wanazoea watu hovyo, watu wamekuja na bajeti zao halafu wewe unawapunguzia. Nitawashauri weny mabendi mengine pia sababu watu wengi wanakimbia bendi zetu kwa sababu ya hilo”, Amesema Zagreb
Zagreb Butamu - Rais wa Akudo
Pia Rais wa Akudo amesema atahakikisha anawashauri viongozi wa band nyingine ili kuweza kuwafanyia kazi wasanii wote wanaopenda kupiga vizinga ili kuweza kuurudisha muziki wa band katika hadhi yake.