
Real Madrid na Liverpool walipokutana kwenye mchezo wa fainali wa Ligi ya mabingwa mwaka 2019
Kwa mara ya mwisho Real Madrid kupoteza mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa ni 27 May, 1981 waliponyukwa na Liverpool bao 1-0 lililopachikwa na Allan Kennedy zikiwa zimesalia dakika 8 mchezo kumalizika.
Baada ya hapo wamecheza fainali 7 kuanzia mwaka 1998 waliifunga Juventus ,2000 wakaitandika Valencia, 2002 waliitandika Bayer Leverkusen,,2014 waliifunga Atletico Madrid,,2016 wakailaza Atletico Madrid,,2017 wakaibwaga Juventus na 2019 wakawalaza Liverpool.
Safari hii Real Madrid itakutana tena na Liverpool katika mchezo wa fainali utakaochezwa 28 May 2022 huko Paris nchini Ufaransa je historia itajirudia au itaendelezwa?
Liverpool ambayo inaingia kwenye fainali ya tatu ndani ya miaka mitano watakutana na Real Madrid ambayo kwa ujumla imepoteza fainali tatu tu kati ya 16 walizocheza, wakishinda 13 na kubeba taji la michuano hiyo mikubwa ya vilabu Ulaya.