
Mshambuliaji wa Mtibwa Salum Kihimbwa akipiga mkwaju wa penati kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Coastal Union
Wenyeji Ruvu Shooting wanaingia kwenye mchezo wa jioni ya leo wakiwa hawajashinda mchezo hata mmoja kwenye michezo 4 ya mwisho ya Ligi Iliyopita, wamefungwa michezo 3 na wametoka sare mchezo mmoja lakini pia wanarejea kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mabatini baada ya kucheza michezo 3 mfululizo ya ugenini.
Kwa upande wa Mtibwa Sugar, kwa mara ya kwanza kikosi hicho kitaongozwa na kocha Salum Shaaban Mayanga ambaye kajiunga na kikosi hicho akitokea Tanzania Prisons. Na kikosi hicho kimeshinda michezo 2 sare michezo 2 na kimefungwa mchezo mmoja kwenye michezo 5 ya mwisho ya Ligi.
Timu hizi zina alama sawa kwenye msimamo wa Ligi zote zikiwa na alama 10 kwenye michezo 11, Mtibwa Sugar wapo nafasi ya 13 juu ya Ruvu Shooting ambao wapo nafasi ya 14, Mtibwa wakiwa na faida ya kufungwa mabao machache ukilinganisha na Ruvu Shooting.