Ijumaa , 6th Jan , 2017

Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa BMT imemshangaa bondia Francis Cheka kwa kudai kuwa haitambui Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC), na kufichua siri kuwa TPBC imekwishasimamia kazi nyingi za bondia za bondia huyo.

Bondia Francis Cheka

Akizungumza na Kipenga ya East Africa Radio, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Mohamed Kiganja amesema TPBC ndiyo iliyomuombea kibali Cheka kwa ajili ya kwenda kwenye pambano lake nchini India, na kwamba Cheka aliwatumia viongozi wa TPBC kwa ajili ya kusainishana mikataba, hivyo ni ajabu kusikia kuwa Cheka haitambui TPBC.

Hivi Karibuni, TPBC ilitangaza kumfungia bondia huyo kwa madai ya kutotimiza masharti ya mkataba wake katika pambano lililokuwa limeandaliwa na promota Kaike Siraju ambapo Cheka aligoma kupanda ulingoni akidai kulipwa pes zake zote kwanza.

Adhabu hiyo ilimfanya Cheka aibuke na kuishangaa TPBC kwa kufanya uamuzi huo, na kudai kuwa yeye hayuko chini ya TPBC, na wala haitambui.

Msikilize hapa Mohamed Kiganja akifafanua uhusiano uliopo kati ya Cheka na TPBC:-

Mohamed Kiganja - Katibu Mtendaji BMT

 

Sauti ya Mohamed Kiganja