Jumatatu , 28th Feb , 2022

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Simba SC imeshuka mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D baada ya kunyukwa mabao 2-0 na RS Berkane jana usiku kwenye mchezo wa raundi ya 3 hatua ya makundi.

Winga wa Simba SC Bernard Morrison

Mabao ya ushindi ya Berkane yamefungwa kipindi cha kwanza ambapo Adama Ba alifunga bao la kwanza dakika ya 32 kabla ya Charki El Bahri kufunga bao la pili dakika ya 41. Takwimu Kwenye mchezo huo zinaonyesha Simba ilipiga mashuti mawili tu  hakuna shuti hata moja lililolenga lango wakati wenyeji wao walipiga mashuti 19 huku mashuti 5 yalilenga goli la Simba.

Kwa kipigo hicho Simba SC imeshuka kutoka nafasi ya kwanza hadi ya pili wakisalia na alama zao 4 kwenye michezo 3, na RS Berkane wamepanda kutoka nafasi ya 3 mpaka ya kwanza wakifikisha alama 6. US Gendamerie wana alama 4 sawa na Simba  wamefikisha alama hizo baada ya kuifunga ASEC Mimosas mabao 2-1, na Asec ndio wanaburuza mkia wakiwa na alama 3.

Michezo ya mzunguko wa 4 ya kundi D itachezwa Machi 11, 2022. Ambapo ASEC Mimosas watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya US Gendamerie na Simba watawaarika RS Berkane jijini Dar es salaam katika dimba la Benjamini Mkapa.