Tanzania yakiri ratiba ngumu

Ijumaa , 12th Jan , 2018

Shirikisho la Riadha Tanzania kupitia kwa katibu mkuu wake Wilhelm Gidabuday limekiri kuwa wanakabiliwa na ratiba ngumu ya michuano ya kimataifa ya riadha kutokana na wingi wa mashindano lakini wanajipanga kufanya vyema.

Gidabuday amesema timu ya wachezaji 15 itaingia kambini tayari kwa kuanza maandalizi ya mashindano ya Dunia ya nusu marathoni, mashindano ya  Jumuiya ya Madola pamoja na mashindano ya riadha ya London.

''Maandalizi ya michuano yote yanaendelea vizuri, tayari waalimu wanawapa mafunzo binafsi wachezaji ambao wameteuliwa kuingia kwenye kambi na kambi itaanza rasmi Januari 15'', amesema Gidabuday.

Katibu huyo pia amesema wanayapa kipaumbele mashindano yote ikiwemo mbio za London kwani ni muhimu kwa nchi huku akikiri kuwa ratiba ya mashindano ni ngumu kwani mashindano yote yatachezwa mwezi April hivyo watawagawa wachezaji ili kupata wawakilishi katika mashindano yote.

Mashindano ya dunia ya Nusu Marathoni yatafanyika Valencia nchini Hispania huku mashindano ya Jumuiya ya madola yatafanyika Austaralia na mashindano ya London yatafanyika jijini humo nchini Uingereza.

Msikilize zaidi Gidabuday kwenye Video hapo chini