
'Serengeti Girls'
Droo ya Kombe la Dunia ilipangwa jana mchana na Tanzania imewekwa kundi moja sambamba na Japan, Canada na Ufaransa.
Serengeti Girls ilifuzu kucheza Kombe la Dunia baada ya kuifunga Cameroon jumla ya mabao 5-1 baada ya raundi ya kwanza mchezo uliochezwa Yaounde, Cameroon kushinda 4-1 na wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar Serengeti ilishinda 1-0 bao likifungwa na Neema Paul Kinega.
Makundi mengine katika Kombe hilo, kundi A India, USA, Morocco na Brazili, Kundi B Ujerumani, Nigeria, Chile na New Zealand.
Kundi C Spain, Colombia, Mexico na China PR.