Simba SC itakua mgeni wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa General Lansana Conte mjini Counakry, saa kumi kwa majira ya nchini Guinea.
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu hiyo ya Msimbazi Ahmed Ally amesema, mipango mikubwa ya Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kocha Roberto Oliveira, ni kuona kikosi chao kinapambana na kupata ushindi ugenin
Ahmed amesema Kocha huyo amekua akiwasisitiza wachezaji wake kuhakikisha hilo linafanikiwa, na kama mambo yatakuwa magumu basi wanapaswa angalau kupata matokeo ya sare ambayo yatakuwa mazuri kwa upande wao.
“Mpango wetu wa kwanza kule Guinea ni kuhakikisha tunapata ushindi. Kama mambo yatakuwa magumu basi tusifungwe na tusishinde.”
“Kiujumla maandalizi mengine ya mchezo wetu wa kwanza wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Horoya AC yanakwenda vizuri.” amesema Ahmed Ally
Wakati Simba SC ikitarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kundi C Jumamosi (Februari 11), Mabingwa wa Soka nchini Morocco Raja Casablanca wataikaribisha Vipers SC mjini Casablanca kwenye Uwanja wa Mfalme Mohammed V Ijumaa (Februari 10), kuanzia saa mbili usiku kwa majira ya Morocco.

